banner

January 19, 2020

SARE YA KUFUNGANA MABAO 2-2 NA CRYSTAL PALACE YAMHUZUNISHA GUARDIOLA, AJA NA GIA NYINGINE

SARE YA KUFUNGANA MABAO 2-2 NA CRYSTAL PALACE YAMHUZUNISHA GUARDIOLA, AJA NA GIA NYINGINE


KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa wana kazi ya kupambana kupata nafasi ya kushirki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa kupata ushindi kwenye mechi zao zilizobaki.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England wameanza kukata tamaa mapema ya kulitetea taji hilo msmu huu baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Crsytal Palace iliyochezwa Uwanja wa Etihad.
Guardiola amesema," Tulifanya kila njia kupata ushindi kwenye mchezo wetu ila bahati mbaya tumepoteza pointi mbili na kuambulia pointi moja hatuna namna nyingine ya kufanya kwani hatukuweza kuzuia mashambulizi ya kushtukiza ya wale vijana.
"Ila ligi inaendelea na tuna mechi nyingi za kucheza. Tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuona kwamba tunapata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao," amesema.
Mabao kwenye mechi hiyo kwa upande wa City yalifungwa na Sergio Arguero kwenye dakika 10 za mwisho ambapo alifunga dakika ya 82 na 87 huku kwa upande wa  Crystal Palace yalifungwa na Cenk Toson dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza na bao la kujifunga kwa City lililofungwa na Fernandinho dakika ya 90 lilitosha kupora ushindi jumla.
Matokeo hayo yanaifanya City kuwa nyuma kwa jumla ya pointi 13 mbele ya vinara wa ligi hiyo Liverpool na wana mechi mbili mkononi za kucheza ambapo leo watacheza na Manchester United.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search