banner

January 19, 2020

SIMBA YATAJA SABABU YA KUIFUNGA ALLIANCE LEO KIRUMBA

SIMBA YATAJA SABABU YA KUIFUNGA ALLIANCE LEO KIRUMBA


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa sababu itakayowafanya Simba waifunge Alliance leo ni kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi yao itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Kagere amehusika kwenye jumla ya mabao 13 ya Simba kati ya 31 akiwa amefunga mabao 10 na kutoa asisti tatu ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi 38 baada ya kucheza mechi 14.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kagere alisema kuwa ligi ina ushindani mkubwa na kila mechi kwao ni muhimu kupata pointi  tatu ambazo ili kuzipata ni lazima kuwafunga wapinzani.
“Kitu pekee ambacho tunakiangalia kwa sasa ni pointi tatu na huwezi kupata pointi tatu bila kufunga ni wakati wetu wa kuendelea kutafuta ushindi ndani ya uwanja jambo litakalotufanya tuwe bora muda wote,” alisema Kagere.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search