Tangaza nasi

February 23, 2020

AZAM FC: KICHAPO CHETU MBELE YA NAMUNGO HATUNA WA KUMLAUMU


AGREY Morris, nahodha wa Azam FC amesema kuwa kichapo walichopokea mbele ya Namungo FC  ni makosa yao wenyewe hakuna wa kumlaumu.

Jana Azam ilipoteza mbele ya Namungo kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Reliants Lusajo dakika ya 60 Uwanja wa Majaliwa.

 Morris amesema:-"Tumefungwa kwa makosa yetu wenyewe hakuna namna nyingine ya kusema wala kumlaumu mtu kwa sasa, ni makosa yetu yamemetugharimu.

Lusajo anafikisha jumla ya mabao 10 wenye msimamo wa wafungaji akiwa ni mzawa mwenye mabao mengi kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara anafuatiwa na Yusuph Mhilu mwenye mabao tisa.


JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka