Tangaza nasi

February 19, 2020

COASTAL UNION YABANWA MBAVU NA RUVU SHOOTING USIKU

MUDHATHIR Said alipachika bao la kuongoza mbele ya Coastal Union dakika ya 50 akiwa ndani ya 18 halikuwazuia Ruvu Shooting kupindua meza kibabe.

Coastal Union, jana Februari 18 ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Ruvu Shooting wakiwa uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani Tanga.

Saadat Mohamed aliweka mzani sawa dakika ya 77, Coastal Union wakiamini kwamba ngoma itakuwa sare walishtuka wakiokota mpira nyavuni dakika za usiku.

Bao la ushindi kwa Ruvu Shooting lilifungwa dakika ya 90 kupitia kwa Graham Naftari na kuwafanya Ruvu Shooting kusepa na pointi tatu jumla.

Matokeo hayo yanaifanya Ruvu Shooting kufikisha jumla ya pointi 32 ikiwa nafasi ya 10 na Coastal Union ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 38.


JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka