banner

February 20, 2020

COASTAL UNION YAWAOMBA RADHI MASHABIKI, HUYU HAPA CHANZO CHA KUPOTEZA MBELE YA RUVU SHOOTING

COASTAL UNION YAWAOMBA RADHI MASHABIKI, HUYU HAPA CHANZO CHA KUPOTEZA MBELE YA RUVU SHOOTING


SUDY Dondola, mlinda mlango namba moja wa Coastal Union amesema kuwa kupoteza pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkwakwani chanzo alikuwa yeye jambo linalomuumiza.

Coastal Union ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao la usiku lililopachikwa na Graham Naftar dakika ya 90 na lile la kusawazisha bao la Coastal Union lililofungwa na Mudhathir Said dakika ya 50 lilifungwa na Sadat Mohamed dakika ya 77.

"Nilikuwa na kazi kubwa ya kulinda lango letu ili tushinde ia mwisho wa siku hesabu zilinigomea jambo ambalo linaniumiza, ninaomba radhi kwa mashabiki wa timu yangu ya Coastal Union.

"Mimi ni mlinda mlango namba moja ninatakiwa kuwa makini muda wote, nimejifunza kupitia makosa na kupoteza Mkwakwani mbele ya mashabiki wetu inauma," amesema.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search