banner

February 19, 2020

LICHA YA KICHAPO CHA MABAO 2-1 MBELE YA MBEYA CITY, DIDA AWEKA REKODI YAKE

LICHA YA KICHAPO CHA MABAO 2-1 MBELE YA MBEYA CITY, DIDA AWEKA REKODI YAKE

MLINDA mlango wa Lipuli ya Iringa, Deogratius Munish 'Dida' anaingia kwenye rekodi ndani ya msimu wa 2019/20 kuwa mlinda mlango wa kwanza kupachika bao ndani ya ligi.

Dida alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti wakati timu yake ikikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City ya Mbeya, Uwanja wa Sokoine.

Mchezo huo ulichezwa Jana, Februari 18 ulishuhudia Lipuli wakiangusha pointi tatu nyingine baada ya kufungwa na Simba bao 1-0 mchezo wao uliopita.

Mabao kwa upande wa Mbeya City yalifungwa na Seleman Ibrahim dakika ya 11 kwa penalti na Peter Mapunda dakika ya 86.

Bao la kufutia machozi kwa Lipuli lilifungwa dakika ya 90+1 na Dida kwa penalti .

Matokeo hayo yanaifanya Lipuli kuwa nafasi ya 12 na pointi 29 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 18 na pointi 21 zote zimecheza mechi 23.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search