Tangaza nasi

February 15, 2020

MHILU ATUMA UJUMBE HUU WA KWA MEDDIE KAGERE

YUSUPH Mhilu, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Kagera Sugar amehusika kwenye mabao 9 kati ya 28, akifunga saba na kutoa pasi mbili za mabao amesema kuwa malengo aliyojiwekea ni kufunga mabao mengi yatakayompa nafasi ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora.
Maneno hayo ni ujumbe kwa kinara wa utupiaji ndani ya ligi, Meddie Kagere anayekipiga Simba akiwa na mabao yake 12 na msimu uliopita alifunga mabao 23.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa kuna kazi kubwa ambayo amejipa ndani ya ligi kufunga kila atakapopata nafasi ili kutwaa tuzo ya mfungaji bora.
“Malengo yangu ni kuona kwamba ninafunga mechi zote nitakazopata nafasi ya kucheza na nafasi ya kufunga, ikishindikana nitatoa pasi za mabao ili kutimiza majukumu yangu ndani ya uwanja, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema Mhilu.


JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka