banner

February 26, 2020

NAMUNGO YACHEKELEA KUTINGA HATUA YA ROBO FAINALI SHIRIKISHO

NAMUNGO YACHEKELEA KUTINGA HATUA YA ROBO FAINALI SHIRIKISHO


NAMUNGO FC jana imetinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa ushindi huo umetokana na wachezaji wake kujituma na kufanya kazi kwa bidii ndani ya uwanja jambo linalomfanya afurahi.

"Ni kazi nzuri vijana wangu wamefanya bado nina imani wataendelea kufanya hivi kwenye mechi zetu zinazofuata.

"Wanatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu ikipata matokeo nao wanapambana kushinda kwa hilo ninawapongeza, " amesema.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search