Tangaza nasi

February 15, 2020

SHIKALO APOTEZWA YANGA, DAKIKA ZATAJWA


KITENDO cha kipa wa Yanga, Metacha Mnata kuanza katika mechi sita mfululizo za Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa na dakika 540, kinachukuliwa kama kumpoteza kabisa kipa mwenzake, Farouk Shikalo kutokana na kushindwa kupata nafasi katika michezo ya hivi karibuni.

Metacha na Shikalo wote walisajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu ambapo Metacha alisajiliwa akitokea Mbao, huku Shikalo akitokea Bandari ya Kenya.

Mwanzoni mwa msimu huu, Metacha na Shikalo walikuwa wakipokezana kuanza chini ya Kocha Mwinyi Zahera na baadaye Charles Mkwasa, lakini imekuwa tofauti kwa kocha wa sasa, Luc Eymael.

Luc tangu aanze kuinoa Yanga, ameiongoza timu hiyo katika michezo nane, saba ikiwa ya ligi kuu na mmoja wa FA.

Katika michezo hiyo, Shikalo alifanikiwa kuanza katika mchezo mmoja tu walipofungwa 1-0 na Azam. Mechi ambazo Metacha amedaka chini ya kocha wa sasa ni; Yanga 0-3 Kagera Sugar, Singida United 1-3 Yanga, Yanga 2-0 Prisons, Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Yanga 2-1 Lipuli, Ruvu Shooting 0-1 Yanga na Yanga 1-1 Mbeya City.


JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka