banner

February 15, 2020

VITA YA MZUNGU NA MZAWA LEO UHURU NI BALAA

VITA YA MZUNGU NA MZAWA LEO UHURU NI BALAA



SAFU ya ushambuliaji wa Azam FC iliyo chini ya Obrey Chirwa mwenye mabao saba imeipoteza safu ya Coastal Union inayoongozwa na Ayoub Lyanga mwenye mabao sita kwa mwezi Februari kwenye mechi nne walizocheza sawa na dakika 360.
Leo Uwanja wa Uhuru saa 10:00 Azam FC inayonolewa na Arstica Cioaba raia wa Romania itakuwa kwenye vita ya kuwania pointi tatu na  Coastal Union inayonolewa na mzawa Juma Mgunda.
Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 44, kwenye mechi za mwezi Februari imefunga jumla ya mabao sita na kufungwa mabao matatu huku ikishinda mechi mbili na kulazimisha sare mbili. Kwenye pointi 12 imebeba nane na kuzipeperusha nne.
 Matokeo yao yalikuwa namna hii:-Mbeya city 1-1 Azam FC, Feb 2, Azam 1-1 Prisons, Feb 5, Azam 3-1 KMC Feb 8, Azam 1-0 Polisi Tanzania.
Kwa upande wa Coastal Union iliyo nafasi ya sita na pointi 34 imefunga mabao matatu na kufungwa mabao matatu kwenye pointi 12 imeambulia pointi tano na kuzipeperusha saba. Matokeo yao yalikuwa hivi:- Simba 2-0 Coastal Union, Februari Mosi, JKT Tanzania 1-1 Coastal, Feb 04, Coastal Union 2-0 Polisi Tanzania, Februari 8, KMC 0-0 Coastal Union Februari 12.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search