Tangaza nasi

March 27, 2020

SUALA LA TSHISHIMBI KUIBUKIA SIMBA, YANGA YATOA TAMKO


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa suala la mchezaji wao Papy Tshishimbi kusepa ndani ya timu hiyo muda utaongea na atafurahia maisha akiwa ndani ya Klabu ya Yanga.


Tshishimbi raia wa Congo ambaye ni nahodha wa Yanga amesema kuwa mkataba wake umebaki miezi minne na amepata ofa nyingi ndani ya Bongo na nje ya nchi huku habari zikieleza kuwa anaweza kuibukia ndani ya Klabu ya Simba.


"Nimesikiliza ofa nyingi na ni kitu ambacho siwezi kuficha unaweza ukasema labda Simba sijui, timu gani nyingine lakini nina ofa nyingi na mkataba wangu wa mwaka mmoja ndani ya Yanga umebakiza miezi minene bado sijasaini mwingine," amesema.


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:-"Umahiri wako,utimilifu wa kazi yako na thamani yako ipo pale palepale Papy Tshishimbi ila muda utaongea na naamini utaendelea kufurahia maisha ukiwa Yanga,".
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka