banner

April 06, 2020

KIBAYA: MUHIMU KUFANYA DUA NA KULINDA KIPAJI

KIBAYA: MUHIMU KUFANYA DUA NA KULINDA KIPAJI

JAFFARY Kibaya nyota anayekipiga ndani ya Mtibwa Sugar amesema kuwa wakati huu wa Virusi vya Corona ni muhimu kwa wachezaji kulinda viwango vyao na kuchukua tahadhari kujilinda.

Kibaya amesema kuwa kwa sasa kila mmoja anapitia kipindi kigumu ila kinachotakiwa ni kutulia na kufuata utaratibu uliowekwa.

"Kipindi cha sasa ni kigumu na kila mtu anahangaika kutafuta faraja na matumaini lakini ni wakati wa kuomba dua kwa kila mmoja ili kila kitu kiwe sawa kirejee kama zamani.

"Kwa upande wa wachezaji ni muhimu kufanya mazoezi binafsi ambayo yatalinda viwango vyao," amesema.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search