banner

April 03, 2020

MHARIRI WA MAGAZETI YA GLOBAL GROUP AWASHUKURU WALIOMTAKIA MEMA SIKU YA KUMBUKIZI YAKE YA KUZALIWA

MHARIRI WA MAGAZETI YA GLOBAL GROUP AWASHUKURU WALIOMTAKIA MEMA SIKU YA KUMBUKIZI YAKE YA KUZALIWA

SIFAEL Paul, mhariri wa Magazeti Pendwa ya Global Group, leo amefanyiwa bonge moja ya 'surprise' na Uongozi wakati akitimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa huku akiwa kwenye nafasi ya uhariri kwa miaka 10. 

Paul kwa sasa anasimamia gazeti la Ijumaa Wikienda ambalo linatinga mtaani kila Jumatatu kwa bei ya shilingi mia nane na Ijumaa ambalo lipo mtaani kila Ijumaa kwa bei ya shilingi 1,000 ambapo amesema kuwa hana la kusema zaidi ya kushukuru kwa wote waliomtakia heri ya kuzaliwa.

Mhariri huyo ambaye amekuwa akifanya kazi kwa weledi akizingatia miiko ya uandishi wa habari alishtushwa na zawadi kibao mezani zilizoletwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo pamoja na keki kubwa ikiwa ni sehemu ya kumpa pongezi ya kumbukizi yake ya kuzaliwa.

Hafla hiyo ilifanywa Makao Makuu ya Global Group, Sinza Mori ambapo wafanyakazi walijumuika pamoja kufurahia na kukata keki na kutoa maneno ya heri kwake.

Saleh Ally ‘Jembe’ amesema kuwa amekuwa akimtazama kwa ukaribu Paul na amegundua kwamba ni mchapakazi muda wote na hagombani na watu bila sababu za msingi.

“Mungu akupe hekima na busara uishi maisha mema, nimekuwa nawe kwa muda wa zaidi ya miaka 10 na sijaona ukiwa ni mgomvi zaidi ya kugombana na watu kwenye masuala ya kazi pekee,” amesema.

Paul amesema kuwa hana kitu kikubwa cha kusema zaidi ya asante kwa wote waliomtakia heri ya kumbukizi ya kuzaliwa.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search