banner

April 03, 2020

PACHA YA BOCCO NA KAGERE ILIANZA KUNOGA

PACHA YA BOCCO NA KAGERE ILIANZA KUNOGA


NAHODHA wa Simba, John Bocco na mshambuliaji Meddie Kagere walianza kutengeneza pacha nzuri kwa kutengeneza urafiki na nyavu kabla ya Ligi Kuu Bara kusimama.

Bocco na Kagere wakati Simba ikiwa imefunga mabao 63 wamehusika kwenye mabao 30 ambapo Kagere amefunga mabao 19 na kutoa  pasi tano za mabao huku Bocco akifunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kwa muda kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Serikali kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilitoa tamko hilo Machi 17.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search