banner

April 06, 2020

YANGA YATOA TAMKO KUHUSU KURUDI KWA MTUPIAJI MAKAMBO

YANGA YATOA TAMKO KUHUSU KURUDI KWA MTUPIAJI MAKAMBO


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mashabiki wanapaswa kuwa na subira kwa wakati huu kuhusu kumrudisha nyota wao wa zamani Heritier Makambo ndani ya Yanga.

Makambo msimu wa 2018/19 alikuwa kinara wa kutupia ndani ya Yanga ambapo alifunga mabao 17 huku kinara wa jumla ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni Meddie Kagere aliyetupia mabao 23.

Kwa sasa imeelezwa kuwa Yanga inamvutia kasi nyota huyo anayekipiga Horoya ili kurejea tena Jangwani.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ni suala la wakati kwa nyota huyo kurejea ndani ya Yanga.

"Mambo bado kwa sasa kwani suala limeanza kuzungumziwa hata dirisha la usajili halijafunguliwa, tunahofia kuvuruga kanuni lakini wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa.

"Makambo tunajua ni kipenzi cha mashabiki wa Yanga na yeye mwenyewe analijua hilo hivyo ikiwa tutamhitaji hakuna tatizo kila kitu kinawezekana," amesema.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search