banner

June 30, 2022

ISHU YA USAJILI WA STRAIKA LA MAGOLI NDANI YA SIMBA LIKITOKEA UGANDA..MAMBO YAMEKUCHA...KAAGA WENZAKE HUKO...

ISHU YA USAJILI WA STRAIKA LA MAGOLI NDANI YA SIMBA LIKITOKEA UGANDA..MAMBO YAMEKUCHA...KAAGA WENZAKE HUKO...


Straika Mkongomani aliyeko kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Simba, Ceasar Manzoki ameaga rasmi wachezaji wenzie na mashabiki wa Vipers ya Uganda.

Taarifa za uhakika zinathibitisha kuwa Simba imefanya mazungumzo na staa huyo wa DR Congo na wameshakubaliana ambapo mkataba wake unamalizika Alhamisi.

Msimu huu kwenye Ligi ya Uganda alitwaa tuzo ya ufungaji bora akiwa na mabao 18, staa wa msimu na mchezaji bora wa wachezaji. Katika ukurasa wake jana aliandika ujumbe wa kuaga akishukuru na kusema hataisahau klabu hiyo.

Mmoja wa viongozi wa Simba alidokeza kwamba mchezaji huyo ndiye mbadala wa Meddie Kagere ambaye watatemana nae. Alisema kwamba Kagere amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Simba lakini lazima wafanye mabadiliko magumu ili kuirejesha Simba kwenye hadhi yake ndani na nje ya Tanzania.

Tayari Simba imeshamtambulisha, Moses Phiri na habari za uhakika ni kwamba anayefuatia ni Manzoki ambaye muda wowote atakanyaga kwenye ardhi ya Tanzania. Winga Mkenya, Harrison Mwenda wameshindwa kuafikiana na amerudi kwao wakati akisikilizia simu ya Azam.



source http://www.sokalabongo.com/2022/06/ishu-ya-usajili-wa-straika-la-magoli.html

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search