banner

September 27, 2022

SIMBA WAMFANYIA KUFRU YA AINA YAKE MGUNDA....AWA KOCHA WA KWANZA MBONGO KUISHI KIZUNGU...APAGAWA KWA FURAHA..

SIMBA WAMFANYIA KUFRU YA AINA YAKE MGUNDA....AWA KOCHA WA KWANZA MBONGO KUISHI KIZUNGU...APAGAWA KWA FURAHA..


Kikosi cha Simba juzi usiku kilikuwa uwanjani kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki visiwani Zanzibar dhidi ya Malindi, lakini mabosi wa klabu hiyo wamemfanyia sapraizi kocha wa mpito, Juma Mgunda aliyekabidhiwa timu hivi karibuni kuchukua nafasi ya Zoran Maki aliyetimkia Al Ittihad ya Misri.

Mabosi wa Simba licha ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja badala ya miezi sita waliopanga mapema kwa kocha huyo aliyemchukua kutoka Coastal Union, lakini wameamua kumtengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zake kwa ufanisi na kuwapa raha mashabiki.

Wakati Mgunda akiongezewa mkataba huo aliambiwa na mabosi hao kuwa, bado wapo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu na ikifanikiwa kupatikana watafanya kazi kwa pamoja bila shida yoyote, lakini wakamuondoa hoteli ya Sea Scape alipofikia awali akitokea Tanga na kumtyafutia nyuma moja ya kifahari iliyopo pembeni mwa fuke ya Bahari ya Hindi eneo la Mbezi Beach.

Nyumba hiyo aliyopewa Mgunda ni ya maana na kifahari kama zile walizokuwa wakikaa makocha waliyowahi kupita Msimbazi akiwamo, Sven Vandenbroeck, Didier Gomes, Pablo Franco na Zoran Maki, kitu ambacho kwa kocha huyo mzawa imekuwa kama sapraizi kwake.

Lakini kama haitoshi inaelezwa mabosi wa Simba katika kutaka kumuonyesha kuna utofauti mkubwa kuinoa Simba na timu nyingine, wakampa gari mpya ya kisasa kabisa aina ya Tata Nexon pamoja na dereva ambayo atakuwa akitumia kwenye mizunguko yake yote ya timu na binafsi.

“Tumeamua kumfanya hata yote kwa lengo la kutaka afanye kazi zake katika mazingira mazuri na rafiki kwani mwanzo alioanza nao umeturidhisha na ujue tuna mechi ngumu za ndani na zile za CAF, hivyo ni lazima kocha asiwe na stresi aua kufanya kazi kwenye mazingira magumu,” alisema mmoja wa vigogo hao wa Simba aliyeomba kuhifadhiwa jina lake.

MSAUZI APIGWA CHINI

Katika hatua nyingine mchakato wa kusaka kocha mkuu mpya unaendelea ukiwa chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez, huku ikielezwa jina la kocha kutoka Afrika Kusini, Cavin Johnson limepigwa chini licha ya kuwa na wasifu nzuri ikiwamo kupata mafanikio akiwa Al Ahly akifanya kazi kama kocha msaidizi chini ya Pitso Mosimane aliyeajiriwa kwa sasa Saudi Arabia.

Inaelezwa, Barbara aliletewa jina la kocha huyo Msauzi na kujiongeza kwa kufanya uchunguzi wake, akiwasiliana na vyanzo vyake mbalimbali Misri alipofanya kazi mara ya mwisho na kupata taarifa ambazo hakupendezewa nazo na hapo hapo alifanya maamuzi ya kuachana naye.

Haikuwekwa wazi kitu gani kilichomponza kocha huyo, lakini Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema mchakato bado unaendelea na hawana haraka ya kukimbizana kutokana na kile kilichokuwa bora ambacho Mgunda amekionyesha ndani ya muda mfupi.

“Mgunda amefanya kazi nzuri na bora ndani tu ya muda mfupi kwa maana hiyo hata viongozi wa juu wanatafuta kocha mpya huku wakiwa hawana presha kubwa kutokana na ubora wa kikosi kwa sasa,” alisema Ally.



source http://www.sokalabongo.com/2022/09/simba-wamfanyia-kufru-ya-aina-yake.html

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search