banner

March 29, 2017

EDEN HAZARD KUNG’OKA KWA PAUNI MILIONI 100

EDEN HAZARD KUNG’OKA KWA PAUNI MILIONI 100

Mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid wapo katika mipango kabambe ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa vinara wa ligi ya England (Chelsea FC) Eden Hazard, ambaye thamani yake inakadiriwa kufikia Pauni milioni 100.
Real Madrid wameripotiwa kutenga kiasi hicho cha pesa kwa lengo la kukata kiu ya kumsajili mchezaji huyo, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa lulu ndani ya kikosi cha Chelsea ambacho kimeonyesha soka safi kwa msimu wa 2016/17.
Aliyewahi kuwa rais wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon, amezungumza na gazeti la The Marca la nchini Hispania na kufichua siri hiyo, ambapo alieleza kuwa, hana shaka na mipango ya klabu yake kwa Hazard.
Hata hivyo Hazard bado ana mkataba na klabu ya Chelsea hadi mwaka 2020, na tayari uongozi wa The Blues umeanza kufanyanae mazungumzo ya kuhakikisha anabaki Stamford Bridge.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search