banner

May 20, 2017

LEO HATUMWI MTOTO DUKANI, TIMU 6 HATARINI KUSHUKA DARAJA

LEO HATUMWI MTOTO DUKANI, TIMU 6 HATARINI KUSHUKA DARAJA

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kufikia tamati leo Jumamosi lakini vurugu kubwa ni kwenye timu zitakazoshuka daraja kuungana na JKT Ruvu.
Hadi kufikia sasa bado timu mbili zitakazoungana na JKT Ruvu hazijajulikana kwa kuwa kuna timu sita ambaoz zipo kwenye nafasi ya kushuka daraja.

Kuanzia timu inayoshika nafasi ya 10 ambayo ni Mbeya City yenye pointi 33, Majimaji ni ya 11 ina pointi 32, African Lyon ya 12 ina pointi 31, Mbao FC ya 13 ina pointi 30, Ndanda FC ya 14 ina pointi 30 na Toto African ni ya 15 ikiwa na pointi 29.

Mechi kali itakuwa Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ambapo Majimaji itacheza na Mbeya City na timu itakayofungwa inaweza kushuka daraja.

Ndanda itakuwa nyumbani kucheza na JKT Ruvu kwenye uwanja wake wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara wakati Prisons itaikaribisha Lyon kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mtibwa Sugar itaikaribisha Toto kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na Mbao FC itacheza na Yanga nyumbani CCM Kirumba, Mwanza na Azam FC itacheza na Kagera Sugar, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search