banner

May 04, 2017

MAMILIONI YA BIKO YAMPANDISHA NDEGE MSHINDI

MAMILIONI YA BIKO YAMPANDISHA NDEGE MSHINDI

Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko Tanzania, Goodhope Heaven (kulia), akimkabidhi mshindi wa Sh Milioni 10 wa bahati nasibu ya kampuni hiyo, Pildas Emmanuel, Dar es Salaam jana.
NA MWANDISHI Wetu,
SHINDANO la bahati nasibu la Biko Ijue Nguvu ya Buku, limezidi kunoga baada ya Pildas Emmanuel mkazi wa jijini Mwanza kukabidhiwa Sh milioni 10.
Mshindi huyo wa tatu aliyepatikana katika droo iliyochezeshwa Jumapili iliyopita, alikabidhiwa zawadi yake juzi jijini Dar es Salaam na kufunguliwa akaunti ya benki ya NMB na kuingiza fedha hizo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na baadhi ya wataalamu wa benki ya NMB kwa ajili ya kumpa elimu ya kifedha mshindi huyo, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema sasa Biko limekolea na wameendelea kumwaga fedha kwa kila mshindi wao, akiwamo Emmanuel aliyeletwa kwa ndege kutoka Mwanza kumkabidhi fedha zake.
Heaven alisema kila siku wamekuwa wakilipa zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh 1,000,000 na zawadi kubwa ya wiki ya Sh milioni 10.
Alisema tayari wamepata washindi watatu huku wakiwa wameshalipa kiasi hicho kwa washindi wawili wengine ambao ni Christopher Mgaya na Nicholaus Mlasu.
“Biko limekolea na linaendelea kuwapatia utajiri Watanzania wanaothubutu kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel, ambao ni mchezo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumalizia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku tiketi moja ikipatikana kwa Sh 1,000.
“Na kila Sh 1,000 itakayolipwa itakuwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh milioni 10, huku mshiriki akiruhusiwa kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi,” alisema Heaven.
Kwa upande wa Emmanuel, alisema kwamba amefurahishwa na huduma zote alizopewa na Biko, ikiwamo ya kumpa fedha zake pamoja na kumleta jijini Dar es Salaam kwa ndege kutoka Mwanza, kwani hakufikiria kutumia usafiri huo katika maisha yake.
“Ingawa nimepata fedha nyingi ambazo sijawahi kuzishika tangu nizaliwe, pia nimeingia kwenye historia kwa sababu na mimi nimepanda ndege.”
Emmanuel aliwasili jijini Jumatatu iliyopita ikiwa ni siku moja baada ya kutangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, katika droo iliyoshuhudiwa pia na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search