banner

May 20, 2017

MBAO FC 1-0 YANGA 'LIVE' FULL TIME, UWANJA WA CCM KIRUMBA, MWANZA

MBAO FC 1-0 YANGA 'LIVE' FULL TIME, UWANJA WA CCM KIRUMBA, MWANZA

FULL TIME
Mbao wanaibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, wanashangilia kwa nguvu kwa kuwa wanajihakikishia kubaki katika Ligi Kuu ya Vodacom.
Dakika ya 96: Mchezo umemalizika, mwamuzi anapuliza kipenga cha kukamilisha kipindi cha pili.
Dakika ya 95: Yanga wanapata kona, inapigwa kona fupi kisha inaingizwa ndani kipa anadaka.
Dakika ya 95: ndikumana yupo chini akipatiwa matibabu. Mchezo unaendelea.
Dakika ya 94: Mchezo unaendelea baada ya kipa kunyanyuka.
Dakika ya 92: Kipa wa Mbao yupo chini baada ya kupamiwa na beki wa Yanga, Bossou wakati Yanga wanashambulia, mchezo umesimama kipa akipatiwa matibabu.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 5 za nyingeza. Kipa wa Mbao anapata kadi ya njano kwa kuchelewesha mpira.
Dakika ya 90: Mbao wamesogea katika lango la Yanga lakini wanakosa mbinu zaidi. Yanga wanapata mpira na kushambulia.
Dakika ya 87: Yanga wanapata kona. Inapigwa na Msuva lakini kipa wa Mbao anauwahi mpira na kuudaka.
Dakika ya 85: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Haruna Niyonzima anaingia Matheo.
Dakika ya 84: Yanga wanaongeza presha, wanalishambulia lango la Mbao lakini wanakosa nafasi wanazopata.
Dakika ya 80: Beki Juma Abdul wa Yanga anapewa kadi ya njani kwa kumchezo mbaya.
Mwamuzi anampa kadi ya njano Simon Msuva kwa kumparamia na kusababishaguke chini.
Wachezaji wa Yanga walimfuata mwamuzi kwa kasi kiasi cha kuanguka chini wakilalamika kuwa mwenzao alichezewa faulo ndani ya eneo la 18 na kipa wa Mbao, walikuwa wakidai penati. Mchezo umesimama kwa muda.
Dakika ya 77: Kunatokea purukushani uwanjani, wachezaji wa Yanga wanamvaa mwamuzi.
Dakika ya 75: Ndikumana wa Mbao anamchezea faulo Martine wa Yanga na inakuwa faulo. Yanga wanaanzisha faulo, wanalisogelea lango la Mbao lakini shuti la Msuva linatoka nje.
Dakika ya 71: Yanga wanapata kona, inapigwa lakini walinzi wanaumiliki, kipa wa Mbao anauwahi mpira na kuudaka.
Dakika ya 69: Yanga wanapata kona, inapigwa lakini Mbao wanaondoa mpira.
Mbao wanafanya mabadiliko, wanamtoa Habib Haji ambaye ni mfungaji wa bao lao , anaingia Rajish Kotecha.
Dakika ya 65: Yanga wanapata nafasi, Emmanuel Martine anabaki yeye na kipa lakini kipa wa Mbao anafanya kazi nzuri.
Dakika ya 64: Inapigwa kona kunatokea vuta nikuvute lakini mpira unaokolewa, inakuwa kona nyingine. Mchezo ni mkali hasa.
Dakika ya 63: Chirwa anachezewa faulo karibu na lango la Mbao, inapigwa faulo, mpira unatoka inakuwa kona.
Dakika ya 58: Yanga wanafanya mabadiliko, wanatoka Zullu na Oscar Joshua, wanaingia Deus Kaseke na Emmanuel Martine.
Wachezaji wa Yanga walifika kwenye lango la Mbao wakati waupigaji kona, wakaanza kufukua kitu kwenye nguzo, ndipo wale wa Mbao wakaanza kuwazuia na kusababisha mzozo uliodumu kwa dakika kadhaa huku mchezo ukiwa umesimama.
Dakika ya 53: Kunatokea mvutano kati ya wachezaji wa Mbao na Yanga. Mzozo ni mkubwa na mchezo umesimama.
Dakika ya 52: Yanga wanaendelea kulishambulia lango la Mbao kwa kasi.
Dakika ya 48: Yanga wameanza kipindi hiki kwa kasi kubwa.
Kipindi cha pili kimeanza.
Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
Tujikumbushe Kikosi Cha Yanga kilichoanza katika mchezo wa leo:
1.Beno Kakolanya 2.Juma Abdul 3.Oscar Joshua 4.Nadri Haroub 5.Vicent Bosou 6.Thaban Kamsoko 7.Simon Msuva 8.Justine Zulu 9.Obrey Chirwa 10.Haruna Niyonzima 11.Geofrey Mwashuya
Tujikumbushe Kikosi Cha Mbao FC kilichoanza katika mchezo wa leo
1.Benedict Haule 2.David Mwassa 3.Asante Kwasi 4.Yusuph Ndikumana 5.Salmin Hoza 6.Jamal Mwambeleko 7. Ibrahim Njohole 8.Pius Buswita 9.George Sangija 10.Boniface Maganga 11.Habibu Haji

MAPUMZIKO
Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza, Mbao wanaongoza bao 1-0, timu zote zimenda vyumbani kupumzika.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Dakika ya 43: Mbao wanatoa upinzani mkali kwa Yanga, wanapata kona mbili mfululizo, lakini mabeki wa Yanga wanakuwa makini na kuondoa hatari.
Dakika ya 39: Yanga wanajibu mapigo, Msuva anapata nafasi lakini kipa anakuwa makini na kuudaka mpira huo.
Dakika ya 37: Mbao wanafanya shambulizi kali, linapigwa shuti linatoka nje kidogo ya lango.
Dakika ya 35: Yanga wanafika langoni, Juma Abdul anapanda kusaidia mashambulizi upande wa kulia.
Dakika ya 30: Yanga wanafika kwenye lango la Mbao mara kadhaa lakini walinzi wa Mbao wanakuwa makini na kuondoa. Shangwe ni nyingi kutoka kwa mashabiki hapa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mitaa ya Kirumba.
Dakika ya 28: Kasi ya mchezo imekuwa kubwa zaidi, Yanga wanapambana kutafuta bao la kusawazisha.
Dakika ya 23: Habib Haji anaipatia Mbao bao la kwanza, amefanya kazi nzuri ya kuwatoka walinzi wa Yanga na kupiga shuti kali lililojaa wavuni. Mbao wanaongoza bao 1-0.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 18: Mpambano ni mkali na una kasi kubwa, Chirwa wa Yanga alipata nafasi ya kukimbia na mpira na kulikaribia lango lakini mpira ukatoka nje.
Dakika ya 14: Kona inapigwa lakini walinzi wa Yanga wanaondoa hatari.
Dakika ya 13: Mbao wanapata kona, lakini kunatokea mvutano baina ya wachezaji wa Mbao na wa Yanga, mwamuzi anazungumza nao na mchezo unaendelea.
Dakika ya 10: Mashabiki ni wengi na kasi ya mchezo inaongezeka.
Dakika ya 5: Mbao wanaendeleza kasi, kipa wa Yanga Beno Kakolanya anakuwa na kazi ya ziada kuwapanga walinzi wake.
Dakika ya 2: Mbao wanafika kwenye lango la Yanga na kufanya shambulizi kali lakini walinzi wa Yanga wanakuwa makini wanaokoa.
Dakika yua 1: Mchezo umeanza kwa kasi.
Mwamuzi anaaznisha mchezo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search