banner

May 24, 2017

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA SAMATTA UBELGIJI

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA SAMATTA UBELGIJI

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Jumanne hii alikuwa jijini Brussels nchini Ubelgiji ambapo akiwa huko amekutana na straika Mtanzania Mbwana Samatta.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Kikwete maarufu kwa jina la JK alionekana akizungumza na Samatta huku picha nyingine Samatta akimkabidhi jezi yake ya Genk.
Kikwete ameandika: "Nikiwa hapa Brussels kuhudhuria Mkutano wa Wadau wa Libya nimepata fursa ya kukutana na mwanasoka na kipenzi chetu Samatta leo hii.
Samatta anaichezea Genk akiwa mshambuliaji wa kikosi cha kwanza katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Hii si mara ya kwanza kwa JK kumtembelea Samatta, akiwa madarakani, aliwahi kumtembelea Samatta na mwenzake, Thomas Ulimwengu wakati wakiwa wanaichezea TP Mazembe ya DR Congo. Kikwete ambaye ni mdau mkubwa wa soka alikuwa katika safari zake za kikazi enzi hizo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search