banner

May 01, 2017

STORI 5 KUBWA NA TETESI ZA USAJILI LEO MEI MOSI, BARCA WAMALIZANA NA SANCHEZ

STORI 5 KUBWA NA TETESI ZA USAJILI LEO MEI MOSI, BARCA WAMALIZANA NA SANCHEZ

Miamba ya soka ya Hispania Barcelona wamefikia makubaliao kumnasa beki wa Ajax Davinson Sanchez na atajiunga mara tu baada ya dirisha la usajili kufunguliwa mwezi Juni.
Barcelona watatoa ada ya uhamisho ya euro 25 milioni ili kumnyakua raia huyo Colombia huyo mwezi Juni. Davinson alisajiliwa na Ajaax akitokea Nacional kwa ada ya uhamisho wa paundi 4.2 milioni.
Barcelona wanamtazama Davinson kama pacha wa baadae wa Samwel Umtiti na mbadala wa Gerrard Pique ambaye umri unaanza kumtupa mkono.
MESSI ANAWEZA KUTUA INTER

Mchezaji wa zamani wa Inter Milan Sandro Mazzola amesema klabu hiyo ina fedha ya kumsajili nyota wa FC Barcelona Lionel Messi.
“Suning ana uwezo wa kumsajili mchezaji anaetaka akiwemo Messi” alisema Mazzola.
Mmoja wa mmiliki anaye wapa nguvu klabu hiyo ni Suning na ana mpango wa kuongezea fedha katika kipindi cha usajili wa majira ya joto mwezi Juni.
Inter imejikuta ikiwa na nguvu ya kujihusisha na kuwasajili nyota kama James Rodriguez, Harry Kane mara baada kutoka katika hali ya matatizo ya kiuchumi na kushuhudia ikimuuza Mateo Kovacic kwenda Real Madrid.
REAL KUMNYAKUA KINDA WA BARCA

Klabu ya Real Madrid inamvizia kinda wa Barcelona Marc Cucurella ambaye mkataba wake unaisha baada ya msimu huu huku kijana huyo akigoma kusaini mkataba mpya.
Cucurella anatazamiwa kuwa moja ya nyota wakubwa baadae kutoka La Masia ila kutokana na beki huyo kufikiria kucheza zaidi ngazi ya juu amegoma kusaini mkataba mpya huku akiangalia uwezekano wa kutimkia klabu nyingine kucheza zaidi.
Madrid wanachukua nafasi hiyo kumshawishi kijana huyo ili aweze kujiunga nao katika majira ya joto ambapo mbali na Real klabu za Chelsea, Man City,Borussia Dortmund na Tottenham Hotspur zinahitaji saini yake.
MATUIDI, BERNARDO SILVA KUTUA UNITED

Nyota wa wawili wa klabu zinazo shiriki ligi ya Ufaransa maarufu kama ‘Ligue 1’ za PSG na AS Monaco Braise Matuidi pamoja na Bernardo Silva wanahitajika na klabu ya Manchester United.
Kwa mujibu wa gazeti la Express linasema United wanajiandaa na ofa ya euro 95 milioni kwa ajili ya viungo hao kutoka Ufaransa. Matudi amekuwa akihusishwa na United tangu majira ya joto yaliopita licha ya kushindwa kufikia makubaliano.
Jose Mourinho yupo katika mpango wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao ili aweze kufanya vizuri katika mashindano na kuweza kurejea katika klabu bingwa barani Ulaya.
HAZARD AMTAKA BATSHUAYI KUTIMKA CHELSEA

Nyota Chelsea Eden Hazard amemsihi Mbelgiji mwenzake Mitchy Batshuayi kutimka klabuni hapo ili kupata timu nyingine na kucheza zaidi ili kuweza kuitwa katika timu ya taifa.
“Anatakiwa kucheza zaidi Chelsea au kutafuta klabu nyingine na kurejea katika kiwango. Alikuwa na msimu mzuri Marseille na alipachika mabao mengi,” Hazard aliiambia tovuti ya Ubelgiji DH.
Batshuayi alitua Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paundi 33 milioni kutoka Marseille na kucheza michezo 17 pekee katika mashindano yote akiwa chaguo la tatu la kocha Antonio Conte.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search