banner

June 02, 2017

STORI KUBWA 6 NA HABARI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUNI 2, MAN U KUFIKIRIA UPYA DAU LA KUMNUNUA GRIEZMAN

STORI KUBWA 6 NA HABARI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUNI 2, MAN U KUFIKIRIA UPYA DAU LA KUMNUNUA GRIEZMAN

KIUNGO ZA ZAMANI WA MAN UNITED, DARREN FLETCHER ASAINI STOKE CITY


Kiungo mkongwe Darren Fletcher amejiunga katika timu ya Stoke City kwa mkataba wa miaka miwili akitokea West Brom.
Fletcher mwenye umri wa miaka 33 ameshindwa kukubaliana na klabu yake hiyo ya zamani baada ya mazungumzo kufanyika tangu msimu huu ulipomalizika.

Mchezaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Manchester United kwa miaka kadhaa anatarajiwa kuanza mazoezi na timu yake hiyo mpya katika mazoezi ya pamoja ya kujiandaa na msimu mpya wa 2017/2018.

MANCHESTER CITY YASAJILI KIPA KWA REKODI YA DUNIA

Timu ya Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Ederson Moraes kutoka Benfica ya Ureno na kuwa usajili wa pili wa Man City baada ya ligi kumalizika.
Uhamisho wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 umeigharimu City kitita cha paundi milioni 35 na kumfanya kuwa kipa wa pili ghali katika historia baada ya Gianliugi Buffon aliposajiliwa na Juventus akitokea Parma mwaka 2001.

Ederson alisafiri kwenda Manchester, Jumatatu na Jumanne alitua katika uwanja wa mazoezi wa City kukamilisha vipimo vya afya na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya klabu.

City sasa wanakuwa wameshatumia kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo kumsajili kumnasa kiungo Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 kutoka Monaco.

YAYA TOURE ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA MAN CITY

Klabu ya Manchester City imethibitisha kumpa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo, kiungo mkongwe Yaya Toure.
Kulikuwa na utata juu ya Yaya kama ataendelea kuichezea timu hiyo kwa kuwa Kocha Pep Guradiola alionyesha wazi kutomkubali katika mwanzoni mwa msimu uliopita lakini baadaye walielewana na kuanza kumchezesha katika kikosi cha kwanza.

MANCHESTER UNITED KUMSAINI NYOTA WA BENFICA VICTOR LINDELOF

Mlinzi wa klabu ya Benfica, Victor Lindelof anatarajiwa kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu ya Manchester United. Mkataba huo wa pauni Milioni 35 unatarajiwa kusainiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili kukamilika.
Siku kadhaa zilizopita gazeti la Kireno  liitwalo O Jogo liliripoti kwamba, raisi wa  Benfica, Luis Filipe Vieira  alisafiri kwenda Uingereza kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili wa mchezaji huyo pamoja na mchezaji mwenzake Nelson Semedo.
Timu nyingine kubwa zinazoonekana kummendea mlinzi huyo ni Real Madrid, Barcelona na New Castle ingawa Jose Mourinho ameonekana pia kumtaka.
Kulingana na O Jogo Rais huyo wa Benfica anaamini kwamba anaweza kuwauza wachezaji hao wawili kwenda Manchester United kwa dau lisilopungua pauni Milioni 83 endapo wakikubali.
Manchester United wamekua wakimtaka Lindelof tokea mwezi wa kwanza mwaka huu lakini uhamisho ulishindikana.
Mourinho ana kazi ya kuandaa kikosi chenye walinzi wazuri kabla ya msimu mpya kuanza tena.

MANCHESTER UNITED KUFIKIRIA UPYA DAU LA ZAIDI YA TSH. BILIONI 247 KUMNUNUA GRIEZMAN

Kuna walakini umejikoteza kwa klabu ya Manchester United kumnunua mchezaji Antonio Griezman wa Atlético Madrid  baada ya  mahakama ya kimataifa ya maamuzi ya kisoka  (The Court of Arbitration for Sport-CAS), kuizuia klabu hiyo kufanya usajili mpaka mwezi wa kwanza mwakani. 
Maamuzi hayo yamekuja kutokana na klabu hiyo ya Hispania kukiuka taratibu kwa kusajili vijana wadogo kinyume na taratibu na yanalenga kuzuia usafirishaji usio halali wa vijana wenye umri mdogo kutoka katika nchi zao.
Kutokana na ukatazwaji huo wa kusajili, endapo klabu hiyo ikimuuza Griezman haitopata mbadala wake.
Atletico Madrid itakubali Kumuuza Griezman endapo tu Manchester United Itakua tayari kutoa Dau la zaidi ya Shilingi Bilioni 247.
Manchester United imekua ikihangaika kutafuta mchezaji atakayecheza No 9 kuziba nafasi ya Zlatan Ibahimovic ambaye ameumia.
Imeelezwa kua endapo Manchester United itamkosa Griezman, chaguo la Kocha Jose Mourinho ni Romelu  Lukaku (24) wa Everton au Alvaro Morata (24)  wa Real Madrid.
Alexandre Lacazette  ndiye mchezaji aliyekua anatumainiwa kuziba pengo la Antonio Griezman endapo angeondoka, lakini ndoto za Diego Simeon zimeonekana kuyeyuka baada ya katazo hilo la mahakama ya kisoka.

IKER CASILLAS AITWA UFARANSA, ANAWEZA KUTUA PSG, MARSEILLE

Kipa mkongwe Iker Casillas kwa sasa anaichezea Porto lakini kumekuwa na taarifa kuwa anaweza kwenda Ufaransa kucheza katika Ligue 1, akiwa anawaniwa na Marseille na Paris Saint-Germain.
Kipa huyo  wa zamani wa Real Madrid ameendelea kuonyesha uwezo wa juu licha ya kuwa umri wake unaonekana kumtupa mkono. 

Tetesi za usajili zinaeleza kuwa timu hizo za Ufaransa zote zinamuwania na zipo tayari kumpa mkataba wa mwaka moja huku malipo ya mshahara wake yakitajwa kuwa yanaweza kuwa euro milioni 5 kwa mwaka.

Casillas kwa sasa ana umri wa miaka 36 lakini hajaonyesha dalili za kustaafu kucheza soka.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search