banner

July 05, 2017

FIFA WASITISHA SAFARI YA KUJA TANZANIA KWENYE KESI YA MALINZI

FIFA WASITISHA SAFARI YA KUJA TANZANIA KWENYE KESI YA MALINZI

Ujumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hautakuja nchini Tanzania baada ya mazungumzo na Kaimu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa njia nya simu.
Karia amesema katika mazungumzo hayo amewaeleza kila kitu kinachoendelea nchini ikiwemo kikao cha leo cha Kamati ya Utendaji na wameridhika na kuitakia kila la heri kamati hiyo.
“FIFA hawatakuja tena, tuliongea nao tukawaeleza kinachoendelea, walitupigia wakitaka kujua kama kulikuwa na muingilio wa serikali katika mchakato, au kama kuna fedha za FIFA zilizotumika vibaya, tukawaambia siyo kweli na kuwaeleza kilichotokea kwa hiyo hawatakuja,” amesema Karia.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search