banner

July 22, 2017

SIMBA USAJILI HUU MAHITAJI YA KOCHA?

SIMBA USAJILI HUU MAHITAJI YA KOCHA?

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog.
KWENYE mitandao ya kijamii mtu mmoja jana alikuwa anapitisha ujumbe kwa njia ya utani akipanga kikosi kizima cha Simba tena kikionekana kuzidi kabisa na wote aliopanga ni wapya.
Utani ule ulikuwa unafanana na ukweli maana wachezaji wapya wanaotajwa ndani ya Simba mpaka jana walikuwa 12, ni sawa na kikosi kipya na wa akiba mmoja. La kujiuliza hapa haya ni mahitaji ya Kocha Joseph Omog au ni kusajili kwa utashi tu, tena wa watu?
Hebu ona utani wa mtu huyu katika mtandao jana alikipanga hivi kikosi cha Simba kuanzia makipa Aishi Manula na Said Mohamed ‘Nduda’, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Salim Mbonde, Yusuf Mlipili, Emmanuel Mseja, Haruna Niyonzima, Jamal Mwambeleko, Ally Shomari, John Bocco na Emmauel Okwi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search