banner

August 23, 2017

AZAM FC: TUMEKAMILIKA TUTAWAPIGA KIMYA KIMYA KISHA KUWA MABINGWA

AZAM FC: TUMEKAMILIKA TUTAWAPIGA KIMYA KIMYA KISHA KUWA MABINGWA

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Nassoro ‘Cheche’ amekizungumzia kikosi chake kuelekea ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom ambapo amedai timu yake ina nafasi kubwa ya kuwa bingwa katika ligi hiyo.
Cheche amesema hayo baada ya kutua salama mkoani Mtwara wakitokea Dar es Salaam, jana kabla ya kuanza kwa ligi hiyo ambapo wao watafungua pazia kwa kukipiga dhidi ya Ndanda FC.
Azam FC itakipiga na Ndanda FC, Jumamosi hii Agosti 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Cheche amesema licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wao, lakini msimu huu wamepanga kufanya vizuri kwa kutoa vipigo kimya kimya akitamba kuanza na Ndanda Jumamosi.
“Sisi hatusemi sana, ila wengi hawana imani na timu yetu ila mwaka huu tutawachapa kimya kimya hadi tunachukua ubingwa na hata Ndanda ambayo inatusumbua wakiwa kwao Mtwara ila wasitegemee kwa mwaka huu.
“Unajua hawa Ndanda kila mwaka wakitupa shida wakikutana na makocha wageni tupu ila mwaka huu mchanganiko wenye timu tumerudi na nina hakika Ndanda kwao wameisha,” alisema.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search