banner

August 14, 2018

WILLIAN AMTOLEA POVU ANTONIO CONTE

WILLIAN AMTOLEA POVU ANTONIO CONTE



Mchezaji wa Chelsea, Willian Borges da Silva amesema kuwa asingekuwa na sababu ya kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo kama aliyekuwa kocha wao, Antonio Conte angesalia kwenye timu hiyo.
Maneno hayo yanadhihirisha wazi kuwa wawili hao hawapikiki chungu kimoja kwani niv kweli kuwa Willian aliamua kuendelea kubaki The Blues mara baada ya Conte kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Maurizio Sarri mapema mwezi Julai.
Alipo ulizwa na juu ya hatma yake ndani ya Chelsea alipokuwa na Conte, Willian alisema asingekuwa na nafasi ya yeye kuendelea kuitumikia timu hiyo na badala yake angefanya maamuzi ya kuondoka.
“Nipo hapa kwa sababu nahitaji kuichezea Chelsea na ningeondoka kama timu hii ingehitaji mimi nifanye hivyo. Kama Antonio Conte angeendelea kubaki ningeamua kuondoka,” alisema.
Klabu za Manchester United na Barcelona zote kwa pamoja zilionyesha nia yakuhitaji huduma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwenye dirisha hili la usajili lililopita hii ni kutokana na Willian kutokuwa na mahusiano azuri na Conte.
Willian amefunga jumla ya mabao 44 katika michezo 238 aliyopata kuitumikia Chelsea tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Anzhi Makhachkala mwaka 2013.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search