Tangaza nasi

October 01, 2018

SIMBA NA YANGA ZAINGIZA MPUNGA HUU TAIFA

Mchezo namba 72 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara(TPL) kati ya Simba na Young Africans uliochezwa Jumapili Septemba 30,2018 Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi milioni 404,549,000.

Mchezo huo ulioanza saa 11 jioni umeingiza jumla ya Watazamaji 50,168.

Mgawanyo wa mapato hayo ni kwenye upande wa VAT, Selcom, TFF, Uwanja, Simba, TPLB, gharama za mchezo, BMT na DRFA.

Kati ya fedha hizo VAT ambayo ni asilimia 18 ni shilingi milioni 61,710,864.41, Selcom milioni 17,901,293.25.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) milioni 16,246,842.12, Uwanja milioni 48,740,526.35.

Wenyeji wa mchezo Simba milioni 194,962,105.41,TPLB milioni 29,244,315.81, gharama ya mchezo 22,745,578.96, BMT milioni 3,249,368.42 na DRFA milioni 9,748,105.27.
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka