Tangaza nasi

December 10, 2018

TFF YAAMUA KUFICHUA SIRI YANGA, YAWATAJA VIRUSI WANAOHARIBU MCHAKATO WA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mchungahela, amewataja viongozi wawili Yanga ambao wanapinga klabu hiyo kufanya uchaguzi.

Mchungahela ambaye amekuwa akiwasiliana na Yanga mara kwa mara kupitia TFF, amewataja watu wawili pekee kusapoti suala hilo na wakiweka nguvu ili uchaguzi ufanyie.

Mwenyekiti huyo amewataja Thobias Lingalangala kuwa ni mmoja ya watu pekee ambao wanahitaji kuona Yanga inafanya uchaguzi wake Januari 13 mwakani il kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Aidha, Mchungahela amesema wengine wote waliosalia wamekuwa wakipinga jambo ambalo linansababisha kuwe na mvutano wa hapa na pale.

Yanga imeamuriwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuhakikisha inafanya uchaguzi wake baada ya nafasi nyingi za uongozi ndani ya klabu kutokuwa na watu.
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka