banner

March 06, 2019

HIZI HAPA ZITAMENYANA ROBO FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO, YANGA KUWAFUATA WAPINZANI WAO MWANZA

HIZI HAPA ZITAMENYANA ROBO FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO, YANGA KUWAFUATA WAPINZANI WAO MWANZA

LEO Droo ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) imefanyika ambapo timu nane zilizotinga hatua ya nane bora zimetambua zitacheza na nani hatua ya robo fainali.

Timu hizo ambazo zilitinga hatua hiyo ni pamoja na Yanga, Alliance FC, African Lyon, Azam FC, Lipuli, KMC na Kagera Sugar.

Michuano hii inatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi itakuwa namna hii:-

 Yanga wataifuata Alliance ya Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba, Kagera Sugar wataikaribisha Azam Uwanja wa Kaitaba.

KMC wataikaribisha African Lyon Uwanja wa Uhuru. 
Lipuli  wataikaribisha Singida United Uwanja wa Samora.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search