banner

May 25, 2019

BIASHARA UNITED YATAJA KILICHOWAKWAMISHA KUBEBA POINTI TATU MBELE YA SIMBA

BIASHARA UNITED YATAJA KILICHOWAKWAMISHA KUBEBA POINTI TATU MBELE YA SIMBA

KOCHA wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa kazi iliyobaki ni kubeba pointi tatu mbele ya Mbeya City kwenye mchezo wake wa mwisho wa ligi utakaochezwa uwanja wa Samora.

Sad leo amelazimisha sare mbele ya Simba kwa kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa na kumfanya asepe na pointi moja.

"Tumepata pointi moja sio mbaya ila tulikuwa tunahitaji pointi tatu, mvua na uwanja leo haukuwa rafiki nawapongeza vijana wangu wameonyesha ushindani na kuwadhibiti wapinzani wao leo.

"Kwa sasa hesabu zangu ni kuelekea mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Mbeya City huo ndio utakaoamua hatma ya timu yangu kubaki kwenye ligi na tunapambana ili tushiriki ligi msimu ujao," amesema.

Biashara United imecheza michezo 37 ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 44 mchezo wake wa mwisho itakuwa ugenini dhidi ya Mbeya City uwanja wa Samora.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search