MANCHESTER United leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Inter Milan mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa wa Singapore.
United imecheza mchezo wa kiushindani na mzuri na walikuwa wakitengeneza nafasi nyingi za wazi.
Mshambuliaji chipukizi Mason Greenwood amezidi kutakata baada ya kufunga bao pekee la ushindi leo.
Huu unakuwa mchezo wake wa pili kufunga kwani hata mchezo wake wa kwanza dhidi ya Leeds alipachika pia bao mshambuliaji huyo mwenye miaka 17.
Post a Comment