Tangaza nasi

January 14, 2020

SIMBA YATAJA KILICHOWAPONZA KUSHINDWA KUTWAA MAPINDUZI, WAJA NA OMBI HILI


JOHN Bocco, nahodha wa timu ya Simba amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda kombe la Mapinduzi mbele ya Mtibwa Sugar.

Simba ilitinga hatua ya fainali kwa kuwatoa mabingwa watetezi Azam FC kwa njia ya penalti 3-2, ilifungwa na Mtibwa Sugar jana, Januari 13 bao 1-0.

"Tunamshukuru Mungu tumemaliza mchezo wetu salama, ila haikuwa bahati yetu kutwaa kombe kwani tulipambana na bahati haikuwa kwetu, tunawaomba mashabiki watupe sapoti kwenye mechi zetu zinazofuata.

"Kwa sasa mpango na nguvu kubwa nakuwa kwenye ligi na mechi nyingine tutafanya vema, pongezi nyingi kwa Mtibwa Sugar," amesema.


JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka