banner

January 19, 2020

SIRI YA AZAM FC KUSHINDA MBELE YA YANGA HII HAPA

SIRI YA AZAM FC KUSHINDA MBELE YA YANGA HII HAPA


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kilichowabeba mbele ya Yanga kwenye mchezo wao wa jana Uwanja wa Taifa ni morali ya wachezaji kucheza bila kuchoka.

Azam FC ilishinda kwa bao 1-0 mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa mbele ya Yanga, bao pekee la Azam FC lilipatikana dakika ya 25 kupitia kwa beki kisiki, Ally Mtoni 'Sonso' ambaye alijifunga katika harakati za kuokoa kona ya Bruce Kangwa iliyopanguliwa na mlinda mlango, Farouk Shikalo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam, Jaffary Maganga amesema kuwa wachezaji walijituma bila kuchoka.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kuwa nafasi ya pili ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 na ina pointi 32.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search