banner

February 22, 2020

CHELSEA V SPURS, LEO NI VITA YA MWANAFUNZI NA MWALIMU

CHELSEA V SPURS, LEO NI VITA YA MWANAFUNZI NA MWALIMU


LEO majira ya saa 9:30 alasiri kutakuwa na vita ya kibabe kwenye Ligi Kuu England kwenye mchezo wa ligi kati ya Chelsea dhidi ya Spurs Uwanja wa Stamford Bridge.

Chelsea iliyo chini ya Frank Lampard ambaye aliwahi kuwa mwanafunzi wa Kocha Mkuu wa Spurs, Jose Mourinho wakati huo akiifundisha Chelsea watakutana kwa mara nyingine tena.

Mchezo wa kwanza walipokutana, mwalimu alizidiwa mbinu na mwanafunzi wake na alichapwa mabao 2-0 hivyo leo itakuwa vita ya kisasi.

Mbinu kali alizotumia mwanafunzi huyo kumshinda mwalimu wake ni kuwatumia mabeki watatu jambo lililoifanya ngome yake kuwa imara.

Vita kubwa ni kutafuta nafasi ya kutinga ndani ya tano bora kwenye msimamo wa Lig Kuu England ili kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chelsea ina pointi 41 kwenye msimamo ikiwa nafasi ya nne huku Spurs ikiwa na pointi 40 nafasi ya tano.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search