banner

February 24, 2020

SIMBA YAWEKA REKODI HII BONGO, YAIACHA YANGA KWA POINTI 21

SIMBA YAWEKA REKODI HII BONGO, YAIACHA YANGA KWA POINTI 21


SIMBA imeweka rekodi yake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa  kuwa ni timu yenye mabao mengi kuliko zote kwa sasa huku ikiwapoteza kwa mbali watani zao wa jadi Yanga.

Simba imefunga mabao 50 kwenye mechi zake 24 ambazo imecheza huku ikiongoza ligi na pointi zake 62.

Watani wao wa jadi Yanga wameachwa nyuma licha ya kuwa na mechi mbili mkononi kwani Yanga imecheza mechi 22 imefunga mabao 25 na ina pointi 41 kibindoni.

Ina deni la pointi 21 ili kuweka mzani sawa huku kwenye upande wa mabao ikidaiwa mabao 25 ili kuweka usawa na Simba yenya mabao 50.

Singida United iliyo nafasi ya 19 ndiyo inayofunga kwenye hesabu za timu zenye mabao machache imecheza mechi 24 na imefunga mabao 13 ikiwa imejikusanyia pointi12.

Kinara wa utupiaji kwa Simba ni Meddie Kagere mwenye mabao 14 na kwa Yanga ni David Molinga mwenye mabao saba.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search