banner

February 14, 2020

YANGA YAWAITA MASHABIKI KESHO TAIFA

YANGA YAWAITA MASHABIKI KESHO TAIFA


JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa timu ya Yanga amesema kuwa ushindani wa Ligi Kuu Bara ni mkubwa nao wanapambana kufikia malengo waliyojiwekea.

Abdul ni kinara wa kutupia pasi za mwisho ndani ya Yanga akiwa ametoa jumla ya pasi nne.

Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa kila mchezaji ana tambua majukumu yake licha ya ugumu ambao wanapitia.

"Ligi ina ushindani mkubwa na kila mchezaji anatambua hilo, ila mwisho wa siku tunapambana kutafuta matokeo mashabiki watupe sapoti ili kufikia malengo tuiyojiwekea," amesema.

Kesho Yanga itamenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa mchezo unaoatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search