banner

October 31, 2020

KAZE AIBUKA NA MBINU MPYA YANGA

KAZE AIBUKA NA MBINU MPYA YANGA

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze hana kazi ya kitoto katika kikosi hicho kutokana na kuibuka na mfumo aliojiwekea wa kuhakikisha anamfanyia tathimini mchezaji mmoja mmoja kwa kumueleza matatizo yake ili kutengeneza kikosi kilicho bora.


Yanga ambayo chini ya Kaze imefanikiwa kushinda michezo miwili mfululizo dhidi ya Polisi Tanzania bao 1-0 na KMC mabao 2-1, leo inatarajia kushuka dimbani kuvaana na Biashara United katika Uwanja wa Karume


Mara huku ikiwa imejiwekea malengo ya kuhakikisha inapata pointi tisa Kanda ya Ziwa.

 

Taarifa ambazo Championi Jumamosi, imezipata kutoka katika benchi la ufundi la Yanga zinasema kuwa, kocha amekuwa na vikao vya mara kwa mara na wachezaji mara baada ya mazoezi na mechi na kuwaambia mapungufu yao mchezaji mmoja mmoja kwa lengo la kujirekebisha.

 

“Mwalimu amekuwa akiwaeleza matatizo wachezaji wake kila baada ya mechi na mazoezi kila mchezaji amekuwa akimwambia mapungufu yake na nini afanye ili kuweza kufanya kile anachokihitaji yeye na hii ndio iliyosababisha timu kuweza kufanya vizuri na kupata mabadiliko kwa haraka.

 

“Kwa jinsi mazoezi yanavyoendelea kufanyika tayari ameshaanza kupata kikosi cha kwanza huku akiwa anaendelea kukifanyia tathimini, amemtaka kila mchezaji kujiona ana umuhimu katika kikosi chake na kujituma ipasavyo ili kufikia malengo ya kupata ushindi katika kila mechi,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Yanga ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa imeshinda michezo sita kati ya saba iliyocheza huku ikitoa sare mchezo mmoja na mpaka sasa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search