banner

May 05, 2021

HAJI MANARA: TUNAIFUNGA YANGA NA UBINGWA TUNACHUKUA

HAJI MANARA: TUNAIFUNGA YANGA NA UBINGWA TUNACHUKUA


OFISA Habari wa Klabu ya soka ya Simba SC, Haji Manara amesema kwasasa ubora wa wachezaji wa Simba ni mkubwa sana ukilinganisha na wachezaji wa Yang na amedai kama kungekuwa na usawa Yanga ingeshuka daraja.

 

Manara ameyasema hayo leo kupitia East Africa Radio alipokuwa akiongea kuhusu kuelekea kwenye mchezo wa watani wa jadi Jumamosi Mei 8, 2021.

 

”Ukitazama wachezaji wa Yanga SC kama kungekuwa na fair wangeshuka daraja, kwasasa wapo nafasi ya pili ni kwasababu ya ukubwa ukubwa tu lakini hawana ubora wa kuifikia Simba SC, iko mbali sana,” amesema Manara.

 

Aidha Manara ameongeza kuwa wamejipanga kuwafunga Yanga na kuchukua ubingwa kabla ya mechi 5 ligi kumalizika kisha wakapambanie ubingwa wa Afrika kwenye klabu bingwa.

 

”Kwanza tunaanza kumfunga Yanga SC kisha tunachukua ubingwa kabla ya mechi 5 za ligi kumalizika kisha tunaenda kushughulikia kombe kubwa Afrika. Hakuna mjadala huu ubingwa wa Tanzania tunachukua miaka 10 mfululizo,” ameeleza.

 

Mchezo huo utarushwa moja kwa moja na Global Radio kuanzia saa 10:00 jioni ambapo utafanyika uchambuzi kabla ya mechi, matangazo ya dakika 45 za kwanza, uchambuzi wakati wa mapumziko, dakika 45 za mwisho na uchambuzi baada ya mechi.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search